Friday, July 19

Tizeba awapa somo wakulima wa pamba

0


Mwanza. Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba amewataka wadau wa pamba kujadili changamoto wanazokumbana nazo zilizosababisha washindwe kufikia malengo msimu wa kilimo uliopita.

Amesema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha changamoto hizo hazijirudii msimu ujao.

Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Novemba 4, 2018 wakati akifungua mkutano wa 14 wa wadau wa sekta ndogo ya pamba jijini Mwanza.

Amesema miongoni mwa mambo aliyoyabaini yanayochangia malengo kutofikiwa ni usimamizi mbovu, kutopata pembejeo kwa wakati hususan viuatilifu na ukosefu wa wataalam katika ngazi za kata.

“Tuangalie tumejikwaa wapi tutoe changamoto zetu za ukweli si za kubuni ili tuone tunatokaje hapa. Tulitarajia kwa msimu huu tuwe wa kwanza barani Afrika katika uzalishaji wa pamba lakini kwa mwendo huu hatuwezi kufika,” amesema Dk Tizeba.

“Ushindani tuliotarajia haukuwepo watu wote walijikita kwenye bei elekezi (Sh1,000 kwa kilo) badala yake hali imekuwa ya kawaida sana nadhani hata haya ni mambo pia ambayo hayataendeleza zao hili.”

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba (TCB), Marco Mutunga amesema malengo yalikuwa ni kupata mavuno tani laki tano lakini zimepatikana tani laki mbili sawa na asilimia 67.

Share.

About Author

Leave A Reply