Saturday, August 24

TFF yapata jezi za Afcon, wapiga mkwara wababaishaji

0


By THOMAS NG’ITU

BAADA ya kelele nyingi kutoka kwa mashabiki wa soka nchini kulalamika kuhusu kukosekana jezi maalum u kwa timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’, Shirikisho la Soka nchini (TFF) tayari wamekata mzizi huo.
Stars inashiriki Fainali za Afcon zinazotarajia kuanza mwezi ujao Juni 21 mwaka huu nchini Misri ambapo haikuwa na jezi zinazotambulika kwa mashabiki wake.
Akizungumza na Wanahabari, Rais wa TFF, Wallace Karia alisema wameamua kukata kiu ya mashabiki baada ya kufanya mazungumzo na kampuni mbalimbali mpaka kufikia kusaini mkataba na kampuni ya Romario Sports 2011 inayotengeneza jezi za Uhlspot.
“Tulizungumza na kampuni za Nike, Umbro, Adidas na Joma lakini tumeamua kumalizana na hawa kwasababu kampuni zingine jezi zao walikuwa wanataka kuwauzia Watanzania takribani dola 25 au Euro 20  ambazo ni sawa na Sh 50,000 mpaka 80,000 isingekuwa rahisi Watanzania wote kupata kwasababu soko  tunalijua,” alisema.
Aliongeza kwamba baada ya kusaini mkataba na kampuni hiyo, wauzaji wengine wa mtaani watahakikisha wanapambana nao ili kuacha kutumia nembo ya TFF kirahisi bila malipo yoyote.
“Mpaka hivi mwenye haki na nembo yetu ni Omario pekee  ambao ndiyo watatengeneza jezi na kusambaza kwa miaka mitatu, hao wengine wa mtaani tunawaambia kabisa tutapambana nao vizuri,” alisema.

Share.

About Author

Leave A Reply