Thursday, August 22

Tarimba awaonya Sevilla, Simba si timu ya mchezomchezo

0


By THOMAS NG’ITU

Dar es Salaam. Mkurugenzi Udhibiti na Utawala wa Sportpesa, Abas Tarimba ameionya Sevilla baada ya kuwaambia mchezo wao dhidi ya Simba wasitegemee kuwa mwepesi hata kidogo.

Akifungua ujio huo alisema anajua kabisa kwamba mpira wa nchini ni tofauti na Hispania, lakini wasitegemee wepesi katika mchezo huo.

“Simba hapa ndio mabingwa wetu kwahiyo katika mchezo hakika hautokuwa mwepesi japokuwa tuna tofauti katika maendeleo ya soka,” alisema.

Tarimba alisema watanzania wameisubili timu hiyo muda mrefu hivyo hategemei kuona kikipangwa kikosi tofauti katika mchezo wao dhidi ya Simba.

“Watanzania wamekuwa wakiwasubili kwa muda mrefu na wote wanajua kwamba mmeshafika, tunatarajia kuona kikosi chenu cha kwanza kikicheza na Simba na sio kikosi kingine,” alisema.

Aliongeza kwa kuwahakikishia Sevilla uwepo wao nchini watakuwa wanafurahia kila dakika ya uwepo wao hapa.

Share.

About Author

Leave A Reply