Sunday, April 21

TAMTHILIA YA SULTAN: Mfahamu Zaina Mziray anayeigiza sauti ya Sah Sultan

0


Deniz Cakır muigizaji wa kituruki ndiye aliyecheza nafasi ya Sah Sultan. Sah katika tamthilia hii ndiye dada wa Sultan, mke wa Lufti Pasha na mama wa Esmehan Sultan ambaye ndio kiboko ya mke wa Sultan, Hurreim kwani unaambiwa hamuogopi kumwambia ukweli pale anapokosea.

Mbali ya kucheza tamthiliya ya Sultan, Deniz pia ameshacheza tamthilya ya “Ferhunde in Yaprak Dokumu na mchezo maarufu wa kuigiza wa Tv nchini Uturuki ulioitwa Eskıya Dunyaya Hukumdar Olmaz kama Meryem Cakırbeyli.

Akiwa na shahada ya masomo ya sosholojia, Zaina Mziray anasema kazi ya kunakilisha sauti si mara yake ya kwanza kuifanya, kwani alishawahi kuifanya katika michezo mbalimbali ya kuigiza katika miradi ya afya ikiwamo ‘Mama Ushauri’.

Pia anasema amesoma masuala ya sanaa ya majukwaani huku matarajio yake ni kujikita zaidi katika tasnia hiyo.

Moja ya sababu ya kutaka kuifanya kazi hiyo ni kutokana na kupata fursa ya kukutana na watu mbalimbali na ni kitu ambacho hujisikia raha kukifanya ukilinganisha na kazi zingine.

Utofauti anaouna kwenye kuingiza sauti, anasema ni muigizaji kutakiwa kufanya vitu vitatu kwa wakati mmoja ikiwamo kuangalia picha, kusoma maneno na kupata hisia.

Lakini kwa sanaa ya jukwaani anasema unakuta script unaisoma na kuifanya kivitendo, hivyo anakiri kunakilisha sio kazi rahisi kama watu wanavyofikiria japokuwa inaweza kuwa rahisi kama mtu unaipenda kazi hiyo kutoka moyoni.

Share.

About Author

Leave A Reply