Sunday, August 25

Staili ya wachezaji Yanga yatua England

0


Baada ya wachezaji wa Yanga kumaliza mgomo wa mazoezi wakishinikiza walipwe mishahara yao, huko England mechi ya Bolton na Brentford Ligi Darajana la Kwanza imeahirishwa jana Ijumaa kutokana na wachezaji wa Bolton kugoma kucheza kutokana na mgomo wakishinikiza kulipwa mishahara yao.

Licha ya mmiliki wa klabu hiyo Laurence Bassini kuwaahidi kuwalipa wachezaji wao malimbikizo ya mishahara yao ili wacheze mechi hiyo jana, hata hivyo walipinga jambo hilo.

Taarifa rasmi iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo imesema kwamba wanaomba radhi kwa kutoelewana huko baina ya wachezaji na uongozi.

Taarifa hiyo, Ilieleza kuwa licha ya tatizo lililojitokeza hatua za kinidhamu huenda zikachukuliwa na Chama cha Soka England kutokana na utovu huo wa nidhamu kwa wachezaji wao.

Hivyo Bodi ya EFL itaamua iwapo kutokana na tatizo hilo lililojitokeza kugoma iwapo mechi itarudiwa au haitakuwapo kabisa.

Hata hivyo, wachezaji wa Bolton walisisitiza msimamo wao wa Ijumaa kwamba, hawatakamilisha ratiba ya mechi zilizosalia msimu huu wala kusafiri kwenda kucheza mechi yao dhidi ya Nottingham Forest mpaka hapo watakapolipwa.

Kigogo Ken Anderson ambaye yupo mbioni kuinunua kabu hiyo, tayari ametoa Pauni 1 milioni kwa ajili ya kuhakikisha malipo ya wachezaji hao yanafanyika mapema kwa sharti kwamba mpango wa kuinunua klabu hiyo ukamilike haraka.

Ligi hiyo yenye timu 24, Bolton ipo nafasi ya 23 ikiwa imecheza  mechi 44 na imekusanya alama 32.

Share.

About Author

Leave A Reply