Saturday, August 17

Simba yazoa alama tatu ikiifunga JKT Tanzania bao 1-0

0


By Olipa Assa

Dar es Salaam. Timu ya Simba imepata bao la usiku na kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Jumanne.

Ushindi huo wa Simba imefikisha alama 72 ikiwa nyuma ya Yanga yenye pointi 77 huku timu hizo zikipunguza uwiano wa pointi ambao sasa ni pointi 5.

Bao hilo la Simba lilifungwa na Hassan Dilunga dakika ya 90+6 na kuwanyanyua mashabiki wa Simba ambao walikuwa wamekata tamaa uwanjani hapo kutokana na piga nikupe kwenye dakika za majeruhi.

Pasi za wachezaji wa Simba nyingi ziliangukia miguuni mwa wapinzani wao JKT Tanzania ambao wanazipa njia zinazowafanya mastaa wa Msimbazi kushindwa kufika gorini. Simba wanatumia mfumo wa 4-3-3.

Kocha Patrick Aussems, alimpanga mbele John Bocco, Emmanual Okwi na Meddie Kagere. Eneo la kati, kiungo mchezeshaji ni Cletous Chama, viungo wakabaji ni Mzamiru Yasin na James Kotei, wakati mabeki wa kati ni Yusuph Mlipili na Erasto Nyoni na mabeki wa pembeni ni Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na Zana Coulibaly.

JKT Tanzania wao walishambulia kwa kushtukiza na kukaba mtu kwa mtu, huku wakiziba njia za Simba kusogea gorini kwao.

Katika harakati za kusaka matokeo kocha Aussems, alimtoa Bocco kisha Chama akapanda juu kusaidiana na kina Kagere na Okwi na Hassan Dilunga aliyeingia anacheza kama kiungo mchezeshaji.

Mabeki wa JKT Tanzania, walitumia nguvu zilizowapa presha washambuliaji wa Simba kukosa utulivu.

Share.

About Author

Leave A Reply