Sunday, August 25

Simba yaivuruga Biashara United mabao 2-0 ikiikaribia Yanga kileleni

0


By OLIPA ASSA

Timu ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Biashara United, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Karume mkoani Mara.

Mbao ya Simba yalifungwa na John Bocco dakika ya 34 na 41 na kuifanya timuhiyo kufikisha alama 69 kwenye msimamo wa Ligi Kuu B
SIMBA inazidi kuisogelea Yanga kileleni baada ya kufanya vyema kwenye mechi zao za viporo, ambapo kwa sasa wamebakiza pointi tano ili kuzifikia 74 za Wanajangwani ambao ndio wameongoza ligi kwa muda mrefu.
Yanga ndio kinara wa ligi kuu Bara kwa pointi 74,wakiwa wamecheza mechi 32, huku watani wao wa jadi Simba wakiwa wamecheza michezo 27 na wamefikisha pointi 69.
John Bocco ndiye alileta amsha amsha kwa timu yake baada ya kufunga mabao mawili kipindi cha kwanza dakika 33 akiambaa na mpira kutoka katikati ya uwanja na kuwapangua mabeki kisha kupiga shuti lililomshinda kipa wa biashara.
Dakika ya 40 Asante Kwasi alimtazama Bocco akiwa ndani ya 18 alimchongea pasi aliyoiunga kwa kichwa na kuipatia Simba bao la pili, hivyo dakika 45 za kipindi cha kwanza Msimbazi walikuwa mbele kwa mabao 2-0.
Mchambuzi wa soka nchini, Ally Mayay alichambua dakika 45 za kipindi cha kwanza za mchezo huo na kusema mbali na Simba kuhitaji pointi tatu muhimu kwao pia ni nafasi kwa washambuliaji wao kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuwania kiatu cha dhahabu kwa msimu huu.
Salim Aiyee wa Mwadui na Meddie Kagera wa Simba ndio wanaongoza kwa mabao 16 mpaka sasa, huku Heritier Makambo wa Yanga akiwa na 15, jambo ambalo Mayay alisema linaleta ushindani na presha kwao kujaribu kutumia nafasi kila mechi ili kupata mabao.
“Mfano John Bocco anazidi kumsogelea Herritie Makambo ambaye ana mabao 15, yeye amefikisha mabao 14 kutoka 14 aliyokuwa nayo na sio huyo tu, Okwi naye anakuja kasi kutoka mabao saba na sasa amefikisha 10, huu ni ushindani wa aina yake”alisema.
Kipindi cha pili timu hizo zilikuwa zinashambuliana kwa zamu ambapo kocha wa Simba, Patrick Aussems alifanya mabadiliko kwa kumtoa Bocco/ Okwi/ Kwasi/ Yusuph Mlipili.
Kabla mechi hiyo kuanza kocha wa Simba, Aussems alisema anawaheshimu Biashara kuwa ni timu ngumu na inacheza kwa kasi “Tunacheza na timu yenye ushindani wa hali ya juu, licha ya kwamba wapo nafasi ya chini ila tutapambana kupata matokeo”alisema.
Naye kocha wa Biashara, Amri Said alisema Simba ni timu yenye wachezaji wazoefu hivyo alitegemea kupata ushindani ya hali ya juu “Kila mechi kwetu tunahitaji kuiheshimu ili kuweza kujikwamua nafasi mbaya tulipo”alisema.

Share.

About Author

Leave A Reply