Tuesday, August 20

Simba Queens wachimba mkwara Mwanza

0


By James Mlaga

Mwanza. Kocha Mkuu wa Simba, Queens Mussa Mgosi ametamba kuwacharaza Marsh Queens kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake utakaopigwa kesho Jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mgosi amesema hayo leo jioni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba wakati timu yake ikifanya mazoezi ya mwisho kuelekea mtanange huo ambao ni mchezo wa mwisho wa   kukamilisha ratiba yao kwa msimu huu.

“Tumejiandaa vizuri kuelekea pambano hilo, Wachezaji wote wapo fiti hivyo sitarajii kumkosa nyota wangu hata mmoja, Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao pia waje kushuhudia burudani safi kutoka kwa Simba,” amesema Mgosi.

Simba inashika nafasi ya pili kwenye mashindano ya Ligi Kuu ya Wanawake ikiwa na alama 44 hivyo kesho wakipata ushindi watakuwa wamefikia malengo yao ya msimu huu ya kumaliza katika tatu bora.Share.

About Author

Leave A Reply