Tuesday, August 20

Shule binafsi zisipambanishwe na za Serikali

0


By Julius Mnganga, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali ameshauri ulinganifu wa matokeo ya shule kwenye matokeo ya kitaifa ufanywe kwa kuzitenganisha shule za Serikali na binafsi.

Kutokana na ulinganifu unaofanywa sasa kila yanapotoka matokeo ya kitaifa, mikoa ya Pwani na Zanzibar imekuwa ikiburuza mkia kila mwaka jambo asiloamini kuwa linamaanisha watoto wengi hawana akili bali namna wanavyolelewa.

“Inawezekana mkoa wa Kilimanjaro unakuwa juu kila mwaka kwa sababu una shule nyingi binafsi tofauti na ya kusini. Lindi tuna shule sita tu binafsi, sidhani kama Pemba zipo,” amesema Bobali.

Ulinganifu wa matokeo hasa ya kidato cha nne na darasa la saba, Lindi na mikoa mingine ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi ikiwamo Mtwara, Pwani, Dar es Salaam na Tanga na visiwa vya Zanzibar hushika nafasi za mwisho.

Bobali anasema wanafunzi hao wakifundishwa madrasa hufaulu vizuri, hivyo haoni sababu za kushindwa masomo yanayofundishwa kwa Kiswahili.

Pamoja na hoja hizo alizozitoa leo Jumanne Aprili 30, 2019 akichangia bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ameitaka Serikali kuangalia kwa kina sababu za baadhi ya mikoa kuendelea kufanya vibaya kila mwaka inapolinganishwa na mingine

Share.

About Author

Leave A Reply