Wednesday, August 21

Shambulizi la kisu laua watatu Japan

0


Tokyo, Japan.  Mtu asiyefahamika amewaua watu wawili akiwamo mwanafunzi msichana baada ya kuwachoma kwa kisu  sehemu mbalimbali za miili yao.

Aidha, katika tukio hilo, watu wengine 17 walijeruhiwa ambako mshambuliaji huyo aliwalenga wanafunzi wa shule waliokuwa wakisubiri basi.

Inadaiwa mshambuliaji huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka ya 50, aliwanyemelea wanafunzi hao kwenye kituo cha basi na kuwachoma visu mara kadhaa kabla ya kujichoma mwenyewe shingoni.

Polisi mjini Tokyo imesema mwanaume huyo alipoteza maisha muda mfupi baada ya tukio hilio.

“Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 11 pamoja na mzazi miaka 39 aliyetambuliwa kuwa ni afisa wa serikali walifariki kwenye shambulizi hilo,” ilisema taarifa hiyo ya polisi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wengi wa waliojeruhiwa ni wanafunzi wenye umri wa miaka 12 ambao walikuwa wakitoka shule kuelekea nyumbani.

Tukio hilo limewastua wananchi wengi wa taifa hilo ambalo visa vya uhalifu wa namna hiyo hutokea kwa mara chache.

Share.

About Author

Leave A Reply