Saturday, August 24

Shabiki wa Real Madrid ashinda Sh208.5 milioni za M-Bet

0


By Imani Makongoro

Dar es Salaam. Shabiki wa Real Madrid, Mkazi wa Ifakara, mkoani Morogoro, Gadi Mwajeka (37), ameshinda Sh 208.5 milioni baada ya kubashiri kwa usahihi mchezo wa Perfect 12 wa kampuni ya M-Bet.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi, Mwajeka alisema hakuamini baada ya kupigiwa simu kuambiwa kushinda kiasi kikubwa cha fedha.

Mwajeka ni mfanyabiashara ya rangi za mkeka Ifakara mjini alisema kuwa ushindi huo ni faraja kubwa kwake kwani utamwezesha kuipanua biashara yake na kuanzisha nyingine.

“Sikuamini kama nimeshinda kiasi kikubwa cha fedha, nimetumia kiasi cha sh1,000 tu kubashiriki na kuingia kiasi kikubwa cha fedha. Nimefarijika sana,” alisema Mwajeka.

Alisema ameshiriki kubashiri muda mrefu mpaka kushinda kiasi kikubwa cha fedha. Amecheza kwa miaka mitatu kucheza na hakukata tamaa.

“Mke wangu ni nesi, nilikuwa nachukua madaftari yake kuandika timu na kuanza kuzipigia mahesabu. Nitatumia fedha hizi kwa ushauri wa wazazi wangu kuona ninafanya biashara gani,” alisema.

Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet, Allen Mushi kuwa Mwajeka ni mshindi wa tano tangu kuanza mwaka huu kushinda zawadi nono.

Mushi alisema M-Bet itaendelea kuwa nyumba ya mabingwa na kuwaomba mashabiki wa soka kubashiri na kampuni yao ili kubadili maisha yao.

“M-Bet ni nyumba za mabingwa na mabingwa wote wanapatikana kupitia michezo ya kubahatisha ya kampuni yetu na kujitajirisha vile vile vile kuichangia nchi yao kwani asilimia 20 ya fedha ukatwa kodi ya kusaidia maendeleo ya nchi katika sekta mbalimbali,” alisema Mushi.

Naye, Shabani Mwanga, Mkuu wa Kitengo cha Kodi za Michezo ya Kubahatisha (TRA), mkoa wa kodi wa Ilala alimpongeza Mwajeka kwa ushindi na pia kuipongeza kampuni ya M-Bet kwa kuwa walipa kodi wazuri kwa serikali.


Share.

About Author

Leave A Reply