Sunday, August 18

Serikali yatumia miaka mitatu kumaliza changamoto mbili za muungano

0


By Sharon Sauwa, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Serikali ya Tanzania imesema kuanzia mwaka 2015 hadi 2019 imetatua changamoto mbili za muungano.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Sima leo Jumanne Aprili 16, 2019, alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Fuoni (CCM) Abbas Ali Hassan Mwinyi.

Mbunge huyo amesema changamoto za muungano bado zipo licha ya vikao vya kamati ya pamoja kati ya Serikali za Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Muungano ya Tanzania (SMT) kukutana mara kwa mara.

“Je ni changamoto zipi zilizopatiwa ufumbuzi tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani? Je ni changamoto hizo ni zipi na ni ngapi?,” amehoji Mwinyi.

Akijibu Sima, amesema hoja zilizopatiwa katika kipindi cha mwaka 2015 hadi mwaka 2019 tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani ni pamoja na ufumbuzi ni utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia.

 Amesema hoja nyingine iliyopatiwa ufumbuzi ni  kutotoza Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa asilimia sifuri kwa umeme unaouzwa na Shirika la Umeme Nchini (Tanesco)  kwa Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco).

Amesema pia kufuta deni lililofikia Sh 22.9 bilioni kwa umeme uliouzwa kwa Zeco.

“Serikali zote mbili ya SMT na SMZ zionaendelea kuhakikisha kuwa makubaliano yaliyofikiwa na pande mbili yanatekelezwa na kuhakikisha kuwa changamoto zinazojitokeza zinashughulikiwa ipasavyo,” amesema.

Share.

About Author

Leave A Reply