Sunday, August 25

Serikali kuboresha mitaala ya elimu

0


Morogoro. Serikali kupitia Wizara za Elimu na Tamisemi imeendelea kuboresha mitaala kwa ajili ya watoto waliokosa elimu kwa mfumo rasmi, ili kuwajengea umahiri pindi wanapohitimu katika ngazi linganishi na mfumo rasmi juu ya ukuzaji wa stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu(KKK).

Aidha, katika uboreshaji huo itahakikisha watoto waliokosa elimu kwa mfumo stahiki wanarudishwa katika mfumo rasmi wapate fursa ya elimu na kama Serikali haitaki kumuacha mtoto yeyote nje ya mfumo.

Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Tickson Nzunda amesema hayo Machi 22 wakati akizungumza na wawezeshaji wa wawezeshaji (TOT) kwenye mafunzo kuhusu uimarishaji wa KKK kwa walimu wanaofundisha madarasa ya Mpango wa Elimu kwa Waliokosa (Memkwa) yanayoendelea mkoani Morogoro.

Nzunda amesema ni vyema walimu hao wakajenga uwajibikaji na usikivu mara baada ya kupata mafunzo ili wawe nyenzo ya kuleta umahiri na kujenga maarifa mapya kwa watoto kuondokana na changamoto

mbalimbali za kukosa fursa ya elimu ya msingi katika umri unaostahili.

Amesema  kwa mujibu wa takwimu za kituo huru cha Serikali zinaonyesha kuwa mwaka 2016 wanafunzi wa Memkwa walikuwa 62,492 kwa nchi nzima, huku mikoa 10 iliyoongoza kwa kuwa nao ni Geita, Kagera, Kigoma, Morogoro, Dar es salaam, Mwanza, Tabora, Rukwa,

Tanga  na Singida na kwamba, ina jumla ya wanafunzi kati ya 2,927 na 8,732.

Mtendaji mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (Adem), Dk Syston Masanja ameeleza kuwa wao kama waratibu wametoa mafunzo kwa wawezeshaji maofisa elimu wa mikoa 26, walimu 1,594 wa Tanzania Bara.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.