Sunday, August 25

Serengeti Boys, Uganda zafuta ndoto kushiriki Kombe la Dunia

0


By Doris Maliyaga

Tanzania U-17 Serengeti Boys imepoteza michezo yote mitatu ya kundi A baada ya kufungwa mabao 4-2 dhidi ya Angola U-17 kwenye mchezo wa fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon)

Mashabiki waliofika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam waliendelea na shangwe kama kawaida licha ya timu hiyo kuonekana kupoteana kimchezo uwanjani.

Vikundi viwili, kimoja jukwaa ambalo hupenda kukaa mashabiki wa Yanga na kingine upande wale wa Simba vimekuwa mstari wa mbele katika kushangilia.

Huu ni mzuka wenyewe wa soka kwani vikundi hivyo ndiyo vimewapa mzuka zaidi mashabiki wengine wanaonekana uwanjani hapa wakiwa mmoja mmoja.

Awali, Serengeti Boys ilikuwa inahitaji ushindi wa manne zaidi mbele ya Angola. Kikosi hicho, ipo Kundi A katika mshindano ya AFCON pamoja na Nigeria, Angola na Uganda.

Mashindano  hayo ya vijana chini ya miaka 17 ya AFCON yanaendelea kutimua vumbi jijini Dar es Salaam na timu mwenyeji ni Serenngeti Boys.

Kwenye Kundi hilo Angola na Nigeria ndizo zimepata nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia baadaye mwaka huu.

Tatizo lilelile la udhaifu wa safu ya ulinzi limeendelea kuitesa Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ katika mechi yake ya mwisho dhidi ya Angola leo kwenye mashindano ya Afrika kwa Vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) inayochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Ukuta huo wa Serengeti Boys umeendelea kuyumba na kuizawadia Angola mabao mawili ambayo yamezidi kuiweka timu hiyo ya vijana ta Tanzania kwenye nafasi ngumu ya kusonga mbele kupitia kundi A licha ya kwenda mapumziko ikiwa sare.

Kosa la kwanza la safu ya ulinzi ya Serengeti Boys ni lile la dakika ya 17 la kumruhusu mchezaji Telson Tome kuruka akiwa mwenyewe kuunganisha mpira wa kona ambao uliipatia Angola bao la kusawazisha.

Bao hilo la kusawazisha la Angola lilikuja ndani ya dakika tano tu baada ya Serengeti Boys kupata bao la utangulizi kupitia kwa Omary Omary aliyefunga mnamo dakika ya 12 akiunganisha mpira wa kona ya Kelvin John.

Dakika ya 41, kiungo Arafat Swakali alifanya makosa ya kizembe kwa kupoteza mpira kwa viungo wa Angola na kisha kucheza faulo ndani ya eneo la hatari ambayo ilisababisha penati iliyofungwa na Osvaldo Capemba Hata hivyo dakika moja kabla ya mapumziko, Agiri Ngoda aliisawazishia Serengeti Boys baada ya kuunganisha vyena pasi ya Kelvin John.

Hata hivyo katika kipindi cha pili, mambo yalizidi kuwa mabaya zaidi kwani uzembe wa kushindwa kumdhibiti winga msumbufu Zito Luvumbo ulizaa bao la tatu kwa Angola mnamo dakika ya 68 baada ya winga huyo kupiga krosi tamu iliyomaliziwa vyema na David Mzanza.

Dakika nne baadaye, Osvaldo Capemba aliwapatia Angola bao la nne kufuatia shambulio la ghafla ambalo timu yake ilifanya baada ya kunasa mpira kutoka kwa viungo wa Serengeti Boys waliokuwa wamepanda mbele kushambulia

Share.

About Author

Leave A Reply