Sunday, August 25

Senegal, Guinea hakuna mbabe

0


 Thobias Sebastian Kipindi cha kwanza kimemalizika kati ya Senegal dhidi ya Guinea hakuna mbabe. Dakika 45, za kipindi cha kwanza katika fainali za mataifa Afrika Afcon ya vijana Senegal walikuwa kwa kwanza kupata bao dakika 9, kupitia kwa Samba Diallo.

Diallo alifunga bao hili kutokana na uzembe wa mabeki wa Guinea kupiga pasi ya nyuma ambayo walishindwa kuikoa.

Kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika timu zote mbili zilikuwa zikishambuliana zamu kwa zamu. Dakika 32, mabeki wa Senegal walishindwa kuokoa pasi ya uchanganishi iliopigwa katika eneo lao na straika Bah Algassime wa Guinea Alison shuti lililotinga nyavuni.

Timu hizi mbili mara baada ya kufungana bao 1-1, ziliendelea kushambuliana kwa zamu lakini hakuna aliyeweza kupata bao la pili ya kuwa na kosa kosa za hapa na pale. Mashindano ya Kombe la Mataifa la Africa (Afcon) ya vijana U 17, yanaendelea hapa nchini na leo ni mechi za mzunguko wa pili katika hatua ya makundi.

Share.

About Author

Leave A Reply