Tuesday, August 20

Sane, Jesus eti wanataka kuondoka

0


Manchester, England. Taarifa za kutoka Hispania zimedai kwamba Leroy Sane na Gabriel Jesus ni mastaa wawili kati ya nane ambao wamedaiwa kuomba kuondoka kwenye kikosi cha Manchester City katika dirisha lijalo la usajili wa majira ya kiangazi huko Ulaya.

Wachezaji hao wote wamekuwa hawapati namba sana katika kikosi hicho kinachonolewa na Pep Guardiola na hilo ndilo linalowataka kuachana na timu hiyo kwenda kutafuta mahali kwingine ambako watapewa nafasi ya kucheza.

Kwa mujibu wa El Chiringuito, kuna wachezaji saba au nane hivi wa Man City ambao wameomba kuondoka katika timu hiyo mwishoni mwa msimu.

Ripoti hizo zimefika mbali kwa kuwataja kabisa wachezaji hao wawili, Sane na Jesus ambao bila shaka Man City wenyewe watapambana kwa nguvu zote kubaki na huduma za wakali wao hao ambao ni muhimu kwa kuwa na umri mdogo na viwango vikubwa.

Jesus ameanzishwa mara nane tu kwenye Ligi Kuu England msimu huu huku akitokea benchi mara 18, wakati Sane amekuwa mwenyeji wa benchi kwa sasa kutokana na kocha Guardiola kuwapendelea zaidi Raheem Sterling na Bernardo Silva.

Share.

About Author

Leave A Reply