Sunday, August 25

Samaki waliovuliwa kwa sumu wateketezwa

0


By Ngollo John, Mwananchi [email protected]

Mwanza.  Zaidi ya kilo 100 za samaki aina ya sato wanaodaiwa kuvuliwa kwa sumu wameteketezwa kwa moto katika ufukwe wa Mswahili jijini Mwanza.

Akizungumza na MCL Digital leo Aprili 22, Mwenyekiti wa Ulinzi wa Rasilimali za Ziwa Victoria (BMU),   Leonard Mpemba amesema samaki hao wamekamatwa leo saa 1:00 asubuhi katika ufukwe wa Chuo cha Ualimu Butimba wakiwa wameshushwa nchi kavu tayari kwa kuuzwa.

“Tulipata taarifa za kuwepo kwa samaki hao na baada ya kufika eneo hilo tulithibitisha kwa kuwashika ambapo walikuwa wanatoka magamba na walikuwa wakinuka harufu ya sumu,” amesema Mpemba.

Boharia wa BMU Mkuyuni, Damian Gabriel amesema baada ya kufika eneo hilo waliwaona wavuvi haramu wakiwa na mapanga na walianza kuwatishia.

“Baada ya kuona hali hiyo nilipiga simu kituo cha Polisi cha Wanamaji (Marine) kuomba askari ambapo walikuja wawili lakini hatukufanikiwa kuwakamata wahalifu kwani walikimbia na kutelekeza samaki hao,” amesema.

Share.

About Author

Leave A Reply