Sunday, August 18

Russia inaitaka Uingereza kupunguza wafanyakazi wake Russia

0
Russia imeiamrisha Uingereza  kupunguza zaidi ya watu 50 kutoka ofisi zake za kidiplomasia na  masuala ya kiufundi huko Russia. Hayo ni madai ya karibuni kutoka Russia katika nyongeza ya ulipizaji kisasi hatua ambayo nchi zote mbili ilizifanya mwanzoni mwa mwezi huu ambapo kila nchi iliagiza kufukuzwa wanadiplomasia wengine 23.

Ijumaa, kremlin ilitoa agizo linalofanana kwa wanadipomasia  59 kutoka nchi 23 za magharibi katika kulipiza kisasi kwa kufukuzwa wanadiplomasia wa Russia kwenye mataifa ya magharibi. Uingereza inaonekana mlengwa kwa kuondolewa idadi kubwa ya wafanyakazi, na balozi wa Uingereza ameambiwa ana mwezi mmoja wa kupunguza wafanyakazi wake kufikia idadi sawa na wafanyakazi wa kidiplomasia wa Russia huko Uingereza.

Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Russia kuwafukuza wanadiplomasia 60 wa Marekani na kufunga ubalozi mdogo wa St.Petersburg. Wawakilishi wa Ujerumani, Uholanzi, Ukraine, Ufaransa, Italy, Poland, Croatia, Ubelgiji, Sweden, Australia, Canada na Jamhuri ya Czech wote walionekana kuwasili katika magari ya kiofisi kwenye jengo la wizara ya mambo ya nchi za nje yaliopo kati kati ya Moscow.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.