Thursday, February 21

Ronaldo: Tumefungwa mabao mepesi sana

0


Turin, Italia. Man United ikiwa ugenini mjini Turin, ilishinda mabao 2-1 na kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ronaldo alisema uzembe wao umewagharimu kwa kuwa walikuwa na nafasi ya kushinda mchezo huo wa jana usiku uliopigwa kwenye Uwanja wa Allianz.

Pia alisema Juventus ilikuwa na uwezo wa kufunga mabao matatu au manne katika mchezo huo uliokuwa na presha kubwa.

“Tulikuwa na uwezo wa kushinda kirahisi kwa kufunga mabao matatu au manne na ana amini kikosi cha Mreno mwenzake Jose Mourinho hakikucheza kwa kiwango bora.

Kikosi cha Kocha Massimiliano Allegri kilijipa matumaini ya kufuzu hatua ya 16 bora, baada ya kutangulia kufunga bao kupitia kwa Ronaldo.

Nyota huyo wa zamani wa timu hiyo, alisema Juventus ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga mabao, lakini ilishindwa kuzitumia.

“Niliangalia mkanda wa marudio. Sikubali kama lilikuwa bao zuri, lakini nilifanya kazi ya ziada kumiliki mpira kabla ya kupiga kiki,” alisema Ronaldo.

Share.

About Author

Leave A Reply