Wednesday, August 21

Real Madrid kuvunja benki kumnasa Neymar

0


Madrid, Hispania. Miamba ya soka la Hispania, Real Madrid inatakiwa kutenga mshahara wa kiasi cha paund 1.2 milioni kwa wiki ili kumshawishi Neymar kuachana na Paris Saint-Germain ya Ufaransa.

Mbrazil huyo, aliyejiunga na PSG mwaka 2017 kwa kuweka rekodi ya dunia ya paund 198milioni, huenda akaondoka kwenye klabu hiyo majira haya ya kiangazi.

Gazeti mashughuli kwa habari ya michezo Hispania (AS), limeandika leo kuhusu kifungu hicho cha fedha ambacho kinaweza kumvutia staa huyo.

Uchanganuzi uliofanywa na gazeti hilo kwa kuzingatia mapato na matumizi ambayo ni kanuni imekuwa ikizingatia kwenye kipindi cha usajili basi Neymar anapishana na Gareth Bale, Real Madrid.

Bale ndiye staa anayetajwa zaidi kuondoka Real Madrid kipindi hiki kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na kocha wa timu hiyo, Zinedin Zidane.

Zidane hakutoa nafasi kwa Bale ya hata kusema kwa kheri kwa mashabiki wa timu hiyo kutokana na kunyima kwake nafasi ya kucheza mchezo wa mwisho wa msimu ambao walipoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Rea Betis.

Mbali na Neymar nyota wengine ambao Zidane anatamani kufanya nao kazi Eden Hazard wa Chelsea, Kylian Mbappe, Christian Eriksen, Paul Pogba na Luka Jovic. 


Share.

About Author

Leave A Reply