Tuesday, March 19

Rais Magufuli kumbe aliwapa dawa Simba kimataifa

0


By OLIPA ASSA

SIMBA wameifanyia kazi kauli ya Rais wa Muungano Tanzania, John  Magufuli, akiwa anawakabidhi ndoo ya ubingwa msimu wa 2017/18 kuwataka waanze kuonyesha kiwango kimataifa.
Rais Magufuli aliwaambia Simba, mwaka huu ambao wanashiriki ligi ya Mabingwa Afrika, wasajili wachezaji wenye viwango vya kuchukua mataji ya kimataifa ili Tanzania iwe na rekodi mpya kwa nchi wanazoshindana nazo.
“Kila timu inayoshiriki ligi ya Mabingwa Afrika lazima ishindwe sasa imefikia hatua awamu hii nataka ushindi Tanzania ni taifa kubwa, TFF mjipange awamu nyingine nahitaji kukabidhi Kombe la Afrika.
“Nimepigiwa kura za kukaa madarakani na wanachama wa Yanga na Simba na wanamichezo wengine, nataka na nyie sasa mfike mbali zaidi kwenye michuano ya kimataifa,”anasema.
Simba imeonyesha kiwango cha hali kuanzia walipocheza Uwanja wa Taifa mechi yao ya kwanza na Mbabane Swallows ambapo waliibuka na ushindi wa mabao 4-1, huku ugenini wakishinda mabao mabao 4-0.

Share.

About Author

Leave A Reply