Saturday, July 20

Rais Madagascar atishia kukataa matokeo

0


Antananarivo, Madagascar. Rais wa zamani wa Madagascar, Hery Rajaonarimampianina amedai chama chake kimegundua dosari nyingi katika uchaguzi mkuu uliofanyika wiki hii hali inayozusha wasiwasi wa kuwepo maandamano na kupinga matokeo ikiwa hataibuka mshindi.
Rajaonarimampianina ambaye alijiuzulu urais Septemba 7 ili ajiandikishe kutetea nafasi hiyo katika uchaguzi uliofanyika Jumatano ametoa malalamiko baada ya matokeo ya awali kutoka baadhi ya vituo kumweka katika nafasi ya tatu nyuma ya wagombea wengine Andry Rajoelina na Marc Ravalamonana ambao wote waliwahi kuwa viongozi wa taifa hilo kwa nyakati tofauti.
Taarifa aliyotoa Rajaonarimampianina Alhamisi jijini Antananarivo imesema uchaguzi huo ulikuwa na dosari za kiufundi na alitaja baadhi kuwa ni kuwepo orodha ya watu waliosajiliwa kimakosa, vitisho na uwepo wa karatasi ambazo tayari zilikuwa zimepigwa kura.
Kiongozi huyo amesema katika taarifa hiyo kwamba hatakubali kuona wananchi wananyang’anywa haki kupitia kura waliyopiga.
Hata hivyo, matamshi yake yanakinzana na yaliyotolewa na waangalizi wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika ambao katika taarifa zao za awali kuhusu uchaguzi huo walisema ulikuwa huru na hapakuwa na dosari kubwa.

Share.

About Author

Leave A Reply