Tuesday, August 20

Rais ataka viongozi kuacha malumbano ya siri

0


By Aurea Simtowe,Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amewataka viongozi wa halmashauri na viongozi wa CCM kuacha malumbano ya kisirisiri katika ufanyaji wa uamuzi.

Ameyasema hayo leo Aprili 29, 2019 katika Halmashauri ya Wilaya ya Busekelo alipokuwa akifungua kipande cha barabara chenye kilomita 10 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika mkoa wa Mbeya.

Amesema kulikuwa na mabishano ya kujenga vituo vya afya baina ya vijiji vitano huku kimoja kikienguliwa kwa kufuata mapendekezo ya vijiji viwili kutumia kituo kimoja kitakachojengwa katikati.

“Sijaona suala la kuweka malumbano hapo kwa sababu kama kila kijiji kitatumia pesa zake kijenge kituo chake.

“Hata mkitaka kuwe na kituo cha afya kila sehemu mjenge  kwa sababu hayo ndiyo maendeleo tunayoyataka, hivyo sioni haja ya nyie kulumbana bali fanyeni vile mnavyotaka,” amesema

Share.

About Author

Leave A Reply