Tuesday, March 19

Raia wa Burundi wauawa wakituhumiwa kupora fedha Sh4milioni

0


By Rehema Matowo Mwananchi [email protected]

Geita. Raia watano wa Burundi wanaotuhumiwa kuwa majambazi wameuawa na wananchi baada ya kuvamia nyumba katika kijiji cha Sungusira kata ya Nzera wilayani Geita na kupora fedha.

Akizungumza leo Jumanne Desemba 4, 2018 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo  amesema tukio hilo limetokea jana Jumatatu Desemba 3, 2018 saa, na  wananchi hao walitumia silaha za jadi kuwashambulia raia hao wa Burundi.

Wanadaiwa kabla ya kuuawa walivamia nyumba za wananchi watatu na kupora Sh4.2milioni.

Katika tukio jingine, watu watatu akiwamo mganga wa kienyeji wanashikiliwa na polisi kwa kukutwa na kichwa cha binadamu.

Walikamatwa Desemba Mosi, 2018  katika Kijiji cha  Rubanga wilayani Geita.

Share.

About Author

Leave A Reply