Tuesday, August 20

Polisi wazingira nyumba ya Bobi Wine

0


Kampala, Uganda. Polisi nchini Uganda wamezingira nyumba ya msanii Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine kumzuia asitoke nje.

Uamuzi huo wa polisi umekuja baada ya Bobi Wine kutangaza kutaka kuwasilisha rasmi barua Polisi kuwafahamisha kuhusu maandamano yake ya amani kupinga kuzuiwa kwa vyanzo vyake vya mapato.

Kikosi cha polisi zaidi ya 50 walizingira nyumba ya mwanamuziki huyo huku wakiwa na silaha pamoja na mabomu ya machozi kwa lengo la kumzuia kutoka nje.

Wine alifikia hatua hiyo baada ya polisi kuzuia tamasha lake kwa madai kwamba hawakuwa na uwezo wa kudhibiti maelfu ya mashabiki wake.

Jana Bobi Wine ambaye ni mbunge wa upinzani, alitiwa nguvuni kwa saa kadhaa baada ya kukamatwa alipokuwa njiani kuelekea kwenye hoteli moja iliyoko iliyopo maeneo ya Ziwa Victoria ambako alikuwa akipanga kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua ya Serikali kumzuia kufanya tamasha lake la Pasaka.

Rais Museveni anasema hatavumilia matamasha yanayochanganywa na siasa.  

Share.

About Author

Leave A Reply