Saturday, August 17

Penalti ya Simba, KMC yawang'oa waamuzi Ligi Kuu

0


By Doris Maliyaga

Dar es Salaam. Waamuzi waliochezesha mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na KMC jana Alhamisi Uwanja wa CCM Kirumba, Abdallah Kambuzi, Godfrey Msakila na Consolata Lazaro, wameondolewa kwenye orodha ya waamuzi wa msimu huu.
Kambuzi alichezesha mchezo huo akiwa mwamuzi wa kati,  wakati mwamuzi msaidizi namba moja alikuwa Msakila na mwamuzi msaidizi namba mbili alichezesha Lazaro na matokeo yalimalizika Simba ikishinda mabao 2-1.
Katika mchezo huo, Kambuzi na wenzake walilalamikiwa na wadau kuchezesha chini ya kiwango hasa katika bao la pili ambalo lilifungwa na John Bocco kwa njia ya mkwaju wa penalti iliyozua utata.

Taarifa hiyo imesema, waamuzi hao wameondolewa baada ya kuonyesha kiwango kisichoridhisha katika mchezo huo uliowakutanisha KMC ikiwa mwenyeji na Simba wageni.

TFF imewaonya waamuzi wa Ligi Kuu Bara kwa kukosa umakini katika uchezeshaji wao na linafuatilia kwa ukaribu mienendo ya waamuzi hao.
Taarifa hiyo, imewaonya pia waamuzi wanaochezesha madaraja ya chini kama Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la pili kwa yeyote atakayebainika kuchezesha chini ya kiwango, atachukuliwa hatua.
S: Waamuzi Abdallah Kambuzi, Godfrey Msakila na Consolata Lazaro wameondolewa kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi Kuu Bara msimu kwa madai ya kuchezesha mechi ya Simba na KMC kwa kiwango kisichoridhisha.

Share.

About Author

Leave A Reply