Thursday, August 22

Pedro ana rekodi za kibabe tu mjini

0


LONDON, ENGLAND.STAA wa Chelsea, Pedro ameandika rekodi mbili baada ya kuisaidia timu hiyo kuichapa Arsenal kwenye fainali ya Europa League.

Katika mchezo huo, Pedro alikuwa miongoni mwa waliotikisa nyavu wakati Chelsea ilipojipigia Arsenal 4-1 na hivyo kubeba ubingwa huo wa Europa League huko mjini Baku, huku wakiwatibulia The Gunners katika kampeni zao za kurudi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Pedro amekuwa Mhispaniola wa kwanza kufunga bao kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, European SuperCup na Europa League, huku akiwa mchezaji wa kwanza pia kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligi Kuu England, Europa League, Kombe la Dunia na michuano ya Euro.

Hata hivyo hayo si mataji yake pekee baada ya kupata mafanikio makubwa pia alipokuwa na kikosi cha Barcelona, ambapo alishinda La Liga, Copa del Rey, UEFA Super Cup na Klabu Bingwa ya Dunia.

Akizungumza baada ya mechi, Pedro mwenye umri wa miaka 31 alisema: “Sasa naweza kustaafu!

“Taji lingine tamu kwa upande wangu. Imekuwa mara ya kwannza kucheza kwenye Europa League na kushinda ubingwa ni kitu spesho. Nimefurahi kufunga nan sasa tunasherehekea pamoja na mashabiki na wale waliostahili. Tumeshinda katika staili nzuri, tumecheza vizuri na tumefunga mabao mengi.”Share.

About Author

Leave A Reply