Friday, August 23

Pauni 400 milioni zafanya kazi, Zidane ataja majembe mapya yakutua Bernabeu

0


MABOSI wa Real Madrid akili zinawacheza kuona mwaka huu wametemeshwa kila kitu kinachoitwa taji. Mbili haikai wala moja.

Kitu cha kwanza walichofanya ni kuwapiga chini makocha, japo walikaa nao muda mfupi. Julen Lopetegui alipigwa chini fasta baada ya timu kufanya vibaya.

Kocha huyo alikuwa kwenye jopo la makocha wa Hispania waliokuwa Russia kwenye Fainali za Kombe la Dunia. Kabla ya Zidane, kocha aliyekuwa na timu ni Santiago Solari.

Hesabu za mabosi zikachekecha, lakini kila wakizungusha ringi, mshale unaangukia kwa Zinedine Zidane ambaye aliondoka na sasa amerejea kikosini baada ya siku 284.

Baada ya kumrudisha, Zidane akawapa masharti ya kwamba baadhi ya wachezaji hawana sifa tena hivyo apate fungu la maana alete mejembe lakini papo hapo uamuzi mgumu ufanyike kuwamwaga wengine.

Kufikia hatua hiyo ni baada ya Real Madrid kushtusha kwa kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa ilipochapwa mabao 4-1 na Ajax Amsterdam na kuifanya timu hiyo ya Uholanzi iliyofuzu kwa jumla ya mabao 5-3.

Zidane alitangaza mapema kwamba lazima Real Madrid ije kivingine, na klabu ikampatia Pauni 400milioni kwa ajili ya kuleta majembe klabuni hapo.

Mtu ambaye anamhangaisha akili na jana alimtaja kwenye listi ya watu wake ni straika wa Chelsea, Eden Hazard pamoja na kiungo wa Tottenham, Christian Eriksen na mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe.

Erikssen ambaye mkataba wake unamalizika, hajamwaga wino Tottenham na ameshawaambia kabisa mabosi wake, anataka kwenda kucheza kwa Zidane.

Kocha huyo anataka kuimarisha kikosi chake ambacho kwa sasa kwenye msimamo wa La Liga kiko nyuma kwa pointi 13 za Barcelona inayoongoza na alisema shughuli nzima itakamilika mwisho wa msimu.

Gazeti la El Confidencial, lilifichua pia kuwa ukiacha Hazard, Zidane anamtaka hata leo, Mbappe atue kikosini. Mbappe, 20, mpaka sasa ana mabao 54 katika mechi 83 alizoitumikia PSG.

Imeelezwa pia kuwa Zidane anamtaka zaidi Mbappe kuliko Neymar lakini pia anamtaka kikosini straika wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann na nyota wa Inter Milan, Mauro Icardi.

Mchezaji mwingine ambaye yuko kwenye listi ya Zidane ni Paul Pogba wa Manchester United na El Confidencial lilifuchua kiungo huyo akili yake ameielekeza Real Madrid.

Akizungumzia ishu ya Paulo Pogba, Zidane alisema: ‘Ninatamani Pogba aje hapa, lakini si kipya nilishalifafanua hili. ‘Ninamfahamu vizuri tu. anaweza kuongeza ladha hapa, ni mmoja wa wachezaji bora dunia hii na anafahamu jinsi ya kushambulia na kuzuia, lakini bado ninaendelea kusaka nyota wengine.

Share.

About Author