Monday, March 18

Papa Francis kufanya ziara UAE

0


Vatican City, Vatican. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis anatarajia kufanya ziara katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Februari 2019 ambako atashiriki mkutano utakaohusisha washiriki wa imani nyingine.
Katika safari hiyo ya kuanzia Februari 3 hadi 5 Abu Dhabi, ujumbe wake utahusu amani, na nembo yake itakuwa na picha ya njiwa aliyebeba tawi la mzaituni. Huko Papa Francis atatoa wito mzito juu ya kuwepo majadiliano baina ya Wakristo na Waislamu na amani katika eneo hilo.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 81 atafanya ziara hiyo wiki moja baada ya kurejea nyumbani akitoka Panama, ambako anatarajiwa kwenda Januari 22 hadi 27 kushiriki katika tamasha la dunia la vijana wa kanisa katoliki.

Share.

About Author

Leave A Reply