Thursday, August 22

Osha yataja sababu kufanyakazi zaidi na sekta binafsi

0


By Yonathan Kossam, mwananchi [email protected]

Mbeya. Mamlaka ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi (Osha) imesema sababu za kufanya kazi zaidi na sekta binafsi ni kutokana na utafiti walioufanya na kubaini sekta binafsi inakabiliwa na changamoto ya usalama mahali pa kazi ikilinganishwa na sekta ya umma.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa usalama na afya mahali pa kazi, Alex Ngata leo Aprili 27 jijini Mbeya katika kongamano la waajiri lililoandaliwa na Osha.

“Huwezi kumlinganisha mtu anayekaa tu ofisini pale wizarani na mfanyakazi wa kiwanda cha chuma mathalani,” amesema.

Ngata amesema sheria inataka watu wote wafikiwe lakini kutokana na uchache wa watumishi walionao wameona ni vema kuanza na maeneo machache wanayoweza kuyafikia.

Mkurugenzi wa Mafunzo, Tafiti, Takwimu na Uhamasishaji Osha, Joshua Matiko amesema kongamano hilo hufanyika kila mwaka kama sehemu ya kuadhimisha kilele cha siku ya afya na usalama mahali pa kazi ambayo huazidhimishwa Aprili 28 kila mwaka.

Kwa upande wake, Nanjela Msangi mshiriki wa kongamano hilo kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) amesema kongamano hilo litawasaidia kuhamasisha wadau kujua na kuzingatia usalama kazini ili kupunguza ajali kazini.

“Sisi kwa mwaka huu tumefurahi kushiriki katika kongamano hili kwani linatupa nafasi kama mfuko kuzungumza na wadau waliopo,” amesema.

Share.

About Author

Leave A Reply