Saturday, August 24

Obafemi adai Nigeria mabingwa Afcon

0


By ELIYA SOLOMON

STRAIKA wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’, Obafemi Martins anaamini taifa lake litachukuwa ubingwa wa fainali za mataifa Afrika nchini Misri zinazotarajia kuanza mwezi ujao.

Martins alikuwa sehemu ya kikosi cha Super Eagles katika fainali za Afcon za mwaka 2006 ambacho kilivaa medali za shaba kama washindi wa tatu na waliitandika Senegal bao 1-0.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Inter Milan katika mahojiano yake, alisema Super Eagles kikosi chao kina wachezaji wenye ubora wa kushinda fainali hizi.

“Wanatakiwa kupewa moyo na wanasaikolojia ili wajione wanaweza kuwa washindi. Pia wanatakiwa kuwa na maandalizi ya kutosha na kingine ni kuwa na namna bora za kimbinu kwenye kutafuta matokeo katika kila mchezo.

“Nikikiangalia kikosi cha maana ya wachezaji wa kizazi hiki wana vipaji vya kuchukua ubingwa wa Afcon, lakini watakutana na ushindani wa kutosha, kikubwa kwao ni kujikita kwenye mipango yao,” alisema.

Mbali na Nigeria kuwapa nafasi, Martins ambaye kwa sasa anaichezea Shanghai Greenland Shenhua FC ya China aliwataja vigogo wengine wa soka la Afrika ambao wananafasi pia ya kutwaa ubingwa wa Afcon, kuwa ni Senegal, Misri , Morocco na mabingwa watetezi, Cameroon.Share.

About Author

Leave A Reply