Tuesday, August 20

Nigeria: Lengo letu tumefanikiwa

0


By THOMAS NG’ITU

KOCHA msaidizi wa timu ya Taifa Nigeria chini ya miaka 17, Bunmi Haruna amesema lengo kubwa katika fainali hizi wamelitimiza baada ya kufanikiwa kufuzu katika kombe la Dunia.

Nigeria walitolewa katika hatua ya makundi na Guinea baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 9-10 huku Angola wakitolewa na Cameroon kwa mikwaju ya penalti 4-3.

 Haruna alisema Taifa lao kiujumla wana furaha baada ya timu yao kufuzu hivyo wamebakisha kipengele kidogo cha kumalizia fainali hizo siku ya kesho.

“Lengo letu tumefanikiwa tayari, lakini mchezo wetu wa kesho bado una umuhimu mkubwa tunaamini kabisa kwamba tunaweza kuibuka na ushindi dhidi ya Angola,” alisema.

Wakati huo huo kocha wa Angola, Pedro Goncalves alisema mchezo wao dhidi ya Nigeria utakuwa mzuri kutokana na kupoteza dhidi yao katika hatua ya makundi.

 “Mchezo utakuwa mzuri lakini pia ni mgumu , tunaoaswa kufanya vizuri na lengo letu ni kuibuka na ushindi,” alisema.

Aliongeza matokeo ya mchezo wao wa nyuma dhidi ya Nigeria hawayafikilii bali wanaangalia mchezo wao wa mbele.

Share.

About Author

Leave A Reply