Sunday, August 25

NIC kuwahakiki wateja wa bima ya maisha

0


By Ephrahim Bahemu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Shirika la Bima Tanzania (NIC) limesema litafanya uhakiki wa wateja wake wa bima ya maisha ili kuboresha huduma na kufanya malipo kwa wanaostahili.

Akizungumza leo Jumanne Aprili 30, 2019 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa NIC, Sam Kamanga amesema mpango huo unaotarajiwa kuanza Juni 3 hadi Julai mosi, 2019 ni utaratibu wa kawaida katika taasisi mbalimbali za fedha.

“Tutafanya uhakiki kupitia ofisi zetu zilizopo mikoa yote, tunataka tuanze kuwalipa wateja halali na kuondoa wateja hewa, bima za maisha ni za muda mrefu hivyo ni muhimu kuwa na maboresho ya taarifa za wateja,” amesema Kamanga ambaye shirika lake sasa lina wateja takriban 300,000.

Kamanga amesema baada ya uhakiki kama kuna malipo hewa yalikuwa yanafanyika yatabainika.

“Katika uhakika mtu atatakiwa kuwasilisha picha zake mbili, taarifa za bima, kitambulisho cha kupiga kura au cha taifa na taarifa za akaunti yake ya benki kwa ajili ya malipo kwa kuwa sasa tunataka kuondokana na malipo ya hundi,” ameema.

Naye kaimu mkurugenzi wa bima za maisha na pensheni wa NIC, Henry Mwalwisi amesema hivi sasa shirika hilo lina wateja zaidi ya 100,000 wa bima ya maisha na uhakiki unafanyika ili kuzuia udanganyifu unaoweza kujitokeza katika sekta ya bima ambako udanganyifu ni mkubwa.

“Tunachukua tahadhari kabla ya hatari lakini hivi sasa kuna mapinduzi makubwa ya teknolojia tofauti na miaka 56 iliyopita, wakati shirika linaanzishwa hivyo tunataka tuhifadhi taarifa za wateja wetu kwa njia za kisasa katika mfumo wa pamoja,” amesema Mwalwisi.

Share.

About Author

Leave A Reply