Tuesday, August 20

Ngoma atoboa siri ya kushindwa kuifunga Yanga

0


By Charity James

Dar es Salaam.Mshambuliaji wa Azam FC, Donald Ngoma ameweka wazi sababu za kushindwa kuifunga timu yake ya zamani Yanga kila wanapokutana nao ni kwa sababu beki wa timu hiyo wanajua ubora na mapungufu yake.

Ngoma tangu ametua Azam FC amefanikiwa kucheza michezo yote miwili ya ligi dhidi ya Yanga, lakini hakuna mchezo hata mmoja aliofanikiwa kufunga.

Ngoma alisema amecheza Yanga misimu miwili na wachezaji wengi waliopo kikosini amecheza nao na kufanya nao mazoezi hivyo wanafahamu mbinu zake na ndio maana mara nyingi kila anapokutana nao amekuwa akionekana hakuna anachokifanya.

“Nikikutana na Yanga nacheza kama ninavyocheza na timu nyingine hakuna ninachokihofia kutoka kwao na katika moja ya michezo ambayo nafurahia kucheza ni kukutana na hiyo timu, lakini kila ninapopambana juhudi zangu hazifanikiwi naamini ni kutokana na kujulikana na nyota wengi ambao nilishawahi kucheza nao,”

“Bado ninanafasi ya kufikia malengo natamani sana kuwafunga ili waweze kutambua kuwa uwezo na upambanaji wangu upo kama nilivyokuwa natua kutoka Zambia nipo sana katika ligi ya Tanzania tukutane msimu ujao,” alisema Ngoma.Share.

About Author

Leave A Reply