Wednesday, August 21

NEC yatangaza ajira uboreshaji daftari la wapiga kura

0


By Mwandishi wetu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza nafasi za kazi za muda kwa ajili ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura.

Kwa mujibu kwa taarifa ya tume hiyo iliyotolewa leo Alhamisi Mei 30, 2019  na kusainiwa na kaimu mkurugenzi wa uchaguzi, Mabamba Moses inaeleza kuwa Watanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na wasiozidi miaka 45 wanaweza kuomba.

Sifa nyingine kwa waomba ajira hao ni kuwa na elimu ya kidato cha nne na kuendelea na ujuzi wa kutumia kompyuta.

“Awe  na uwezo wa kutambua matatizo ya kompyuta ya hardware na software na kuyatatua. Awe na uwezo wa kuweka programu za kompyuta na kutoa msaada wa kuifundi wa Tehama kwa watumiaji.”

“Awe hajawahi kutiwa hatiani kwa makosa ya jinai na  awe na uwezo wa kufanya kazi katika mazingira yenye usimamizi mdogo,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Share.

About Author

Leave A Reply