Sunday, August 25

Mzungu wa Angola azungumza Kiswahili

0


By Doris Maliyaga

 Dar es Salaam. Kocha wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Angola, Pedro Valdemar amekinasa Kiswahili baada ya kukiongea kwenye ukumbi wa habari.

Pedro ambaye ni Mreno alikiongea baada ya timu yake kuibuka washindi wa tatu wa michuano ya AFCON yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Baada ya kukaribishwa katika ukumbi huo, Pedro ambaye anazungumza Kiingereza na Kireno, alishukuru kwa Kiingereza na baadaye akasema Asante akishukuru kwa Kiswahili.

Hiyo ni jambo la kipekee na zuri kwa Watanzania kama ambavyo kauli ya Rais wa Jamhuri ya Tanzania, John Magufuli kusisitiza Lugha ya Kiswahili izungumzwe kila mahali.

Kwa Pedro haikuwa lazima kwake kushukuru Kiswahili isipokuwa alivutiwa tu akazungumza. Fainali za AFCON zilishirikisha timu nane lakini makocha walitumia lugha zao kujieleza. Hata hivyo, baadaye Pedro amesema, amefurahi kuishi Tanzania na amevutiwa kutokana na namna wanavyojua mpira wa miguu.

“Sikuwa najua Tanzania kabla na sikuwa naisikia hivyo ilikuwa mara ya kwanza kufika. Nilikuwa naielewa tofauti na namna nilivyoikuta. Nilijua ni nchi ambayo ipo ipo tu lakini imenivutia kwa kiasi kikubwa,”alisema Pedro.

Kocha wa Nigeria alisema, tangu amefika Watanzania walitaka azungumze Kiswahili lakini aliwaambia hajui.

Share.

About Author

Leave A Reply