Monday, August 26

Mwanamke aua jambazi kwa kisu

0


Nairobi,Kenya. Mwanamke mmoja ameua jambazi mmoja kwa kisu kati ya wawili waliovamia duka lake.

Tukio hilo limetokea saa 9:00 Alhamisi katika eneo la Ngangarithi, Nyeri nchini Kenya.

Polisi wamesema majambazi hao yalivunja duka wakiwa na silaha na kuiba vitu kadhaa ambavyo walivificha katika kichaka karibu na eneo hilo.

Mtandao wa gazeti la Nation umeleeza kuwa, mume wa mwanamke huyo amesema walipigiwa simu na jirani mmoja wa eneo hilo kuwa duka lao limevunjwa na wao wakakimbilia eneo la tukio na walipofika walikutana majambazi ambao wamekimbilia uelekeo tofauti.

Mume na majirani walimkimbiza mmoja wao wakimuacha mwanamke katika eneo la duka.

Baada ya muda, yule jambazi mwingine anayedaiwa kuwa alikuwa amejificha karibu na duka hilo alirudia pale dukani na kujaribu kumbaka yule mwanamke.

Katika purukushani mwanamke alifanikiwa kupata kisu na kumchoma jambazi shingoni. Alifanikiwa kukimbia lakini akaanguka na kupoteza maisha mita kadhaa kutoka dukani.

“Ni kweli  kulikuwa na tukio kama hilo asubuhi hii. Bado tunaandaa taarifa na tutatoa taarifa baadaye,” amesema Kamanda wa Polisi wa Kituo cha Nyeri, Bernard Amugune.

Polisi wamesema wamefanikiwa kupata vitu vilivyokuwa vimeibwa huku wakiendelea kumsaka jambazi mwingine. Mwili wa marehemu umepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Nyeri.

Share.

About Author

Leave A Reply