Friday, July 19

Mwanamfalme aliamuru Khashoggi auawe – CIA

0


Washington, Marekani. Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) limekamilisha uchunguzi wake kwa kusema mwanafalme Mohammed bin Salman ndiye aliamuru mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi katika ubalozi wake mdogo wa Istanbul, Uturuki, vimeripoti vyombo vya habari Ijumaa.

Maelezo haya yanakinzana na madai ambayo yamekuwa yakitolewa na utawala wa Saudi Arabia kwamba mrithi huyo wa ufalme hakuhusika.

Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post, ambalo lilikuwa la kwanza kuripoti kukamilika kwa uchunguzi wa CIA, maofisa wa Marekani wameelezea kuridhishwa na tathmini ya CIA ambayo ni ya uhakika kwa sasa inayomhusisha bin Salman katika mauaji na inatatiza juhudi za Rais Donald Trump ya kuhifadhi uhusiano na mmoja wa washirika wa karibu wa Marekani katika ukanda.

Magazeti yote mawili – Washington Post na Associated Press – yalinukuu maofisa ambao hawakutajwa majina yao lakini wanaofahamu hitimisho la CIA. Usahihi wa ripoti haukuweza kuthibitishwa mara moja.

Ikulu ya White House ilikataa kutoa maoni juu ya ripoti ya Post, ikisema hilo lilikuwa suala la intelejensia. Wizara ya Sheria na maofisa wa CIA pia walikataa kutoa maoni yao.

Khashoggi, mwandishi wa safu maalum katika gazeti la Washington Post, aliuawa katika ubalozi mdogo wa Saudia ulioko jijini Istanbul Oktoba 2 alipokwenda kuchukua nyaraka zilizokuwa zinahitajika kwa ajili yandoa yake.

Mkosoaji huyo wa serikali ya Saudi, Khashoggi alikuwa amekataa shinikizo la Saudia kumtaka arudi nyumbani.

Awali Saudi Arabia ilikanusha madai ya maofisa wake kuhusika na mauaji hayo, lakini kadri mamlaka za Uturuki zilivyoendelea kushupalia na kuvujisha ushahidi wa maofisa wa ngazi ya juu kuhusika, hatimaye utawala ulikiri kwamba mawakala wake walihusika katika mauaji huku ukitoa maelezo yanayokinzana.

Maofisa wa Uturuki walisema kwamba mauaji hayo yalikuwa yamepangwa na wamekuwa wakishinikiza utawala wa Saudia kuwakamata na kuwarejesha ili wakabiliwe na mashtaka. Mshauri wa Rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan Alhamisi aliishutumu Saudi Arabia kwa kujaribu kufunika mauaji hayo.

Matamshi yake yalikuja muda mfupi baada ya naibu nwendesha mashtaka mkuu wa Saudia, Shaalan al-Shaalan kusema alikuwa anapendekeza adhabu ya kifo kwa washukiwa watano wa mauaji ya Khashoggi. Al-Shaalan aliwaambia waandishi wa habari kwamba mwanafalme hakuwa anajua chochote kuhusiana na operesheni hiyo ambayo ilihusika na kuukatakata mwili wa Khashoggi na kuuondoa kutoka majengo ya ubalozi.

Balozi wa Saudia ahusishwa

Ripoti ya Ijumaa kwenye gazeti la Washington Post, ambayo ilinukuu watu wenye ufahamu na suala hilo, ilisema CIA walifikia hitimisho baada ya kufanyia uchunguzi vyanzo mbalimbali vya intelejensia zikiwemo simu zilizopigwa ikiwemo ya kaka wa mwanamfalme Khalid bin, balozi wa Saudia nchini Marekani,n aliyompigia Khashoggi.

Khalid alimwambia Khashoggi lazima aende kwenye ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul kuchukua nyaraka na alimhakikishia kwamba itakuwa salama kufanya hivyo, liliandika gazeti hilo.

Washington Post, likinukuu watu wenye ufahamua na simu zilizopigwa, lilisema hakukuwa na uhakika ikiwa Khalid alifahamu Khashoggi anakwenda kuuawa lakini inafahamika alipiga simu kwa maelekezo ya kaka yake.

Balozi Khalid bin Salman alisema kwa njia ya Twitter Ijumaa kwamba mara ya mwisho aliwasiliana na Khashoggi kwa ujumbe mfupi wa siku Oktoba 26, 2017, karibu mwaka mmoja kabla ya mwanahabari huyo kukutana na kifo.

Mazishi ya Khashoggi

Mazishi ya Khashoggi yalifanyika Makka na Medina na pia hapa Uturuki bila ya uwepo wa mwili wake, ambao hadi sasa haujulikani ulipo.

Kikundi cha waandishi wa habari wa Uturuki kilifanya ibada ya mazishi katika msikiti uliopo jijini Istanbul Ijumaa. Waombolezaji wengi waliswali kumuombea Khashoggi, ambaye aliuawa mwezi Oktoba katika ofisi za ubalozi mdogo wa Saudi Arabia zilizopo nchini Uturuki.

Yashin Aktay, ambaye ni mshauri wa Rais Recep Tayip Erdogan wa Uturuki, alisema serikali ya Uturuki itaendelea kuhoji mhusika halisi wa kosa hilo ni nani, na mwili wa mwanahabari huyo upo wapi.

Juzi Alhamisi, waendesha mashitaka nchini Saudi Arabia waliwashitaki watu 11 kwa madai ya kuhusika na mauaji hayo. Pia walikanusha kuhusika kwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman katika kesi hiyo.

Serikali ya Uturuki inasema sehemu ya taarifa iliyotolewa na waendesha mashitaka hao haitoshelezi.

Rafiki wa Khashoggi aliyehudhuria ibada hiyo ya mazishi alisema maelezo ya mamlaka za Saudi Arabia hayana tija, na alizitaka mamlaka hizo kuweka bayana mtu aliyetoa amri ya kufanyika mauaji hayo.

ndani ya siku saba.

Kuhusu tatizo hilo kuanza kughubikwa na vitendo vya rushwa, alikiri mazingira hayo kuweza kutokea lakini, akasema kuwa hakuna tukio lililoripotiwa ama kugundulika akiwatahadharisha wananchi kutojiingiza kwenye mazingira hayo.Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Kamishina mkuu wa Uhamiaji alisema tatizo hilo litaendelea hadi mwishoni mwa Aprili.

“Kutokana na kuchelewa kuwasili nchini malighafi kwa ajili ya kuchapisha pasipoti hizo, maombi yote ya pasipoti yatakayoshughulikiwa kwa haraka ni yale ya waombaji wenye ushahidi wa safari za dharura nje ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki,” alisema taarifa hiyo na kuongeza:

Kwa wale wenye safari za ndani ya nchi za Jumuiya ya Mashariki, wanashauriwa kuomba pasipoti ya Afrika Mashariki kwa gharama ya Sh15,000 au shahada ya dharura kwa gharama ya Sh10,000 na maombi yao yatashughulikiwa kwa wakati.”

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, waombaji wa pasipoti wasiokuwa na safari za haraka, maombi yao yatashughulikiwa baada ya kuwasili malighafi hizo, mwishoni mwa mwezi Aprili 2012.

“Tunawatahadharisha wananchi kuwa makini na baadhi ya watu wanaoweza kutumia hali hii kufanya vitendo vya utapeli au kuomba rushwa kwa madai ya kuwasaidia kupata pasipoti kwa urahisi zaidi,” alisema na kuongeza:

“Ada ya huduma ya pasipoti ya kawaida ni Sh50,000 tu na inalipwa na mwombaji kupitia benki baada ya ombi lake kupokelewa na Ofisa anayehusika ofisini.”

Share.

About Author

Leave A Reply