Tuesday, August 20

Msimu wa pamba kuanza kesho, walanguzi waonywa

0


By Habel Chidawali, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Serikali ya Tanzania imewaonya walanguzi wa pamba ambao wameanza kununua zao hilo kabla ya msimu uliopangwa.

Onyo hilo limetolewa bungeni leo Jumanne Aprili 30 na Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa ambaye amesema Serikali imejiandaa kikamilifu katika msimu huu.

Naibu waziri huyo alikuwa anajibu swali la nyongeza la Mbunge wa Sumve (CCM), Richard Ndassa ambaye amesema kwa sasa wakulima wa pamba wanalanguliwa kwa bei ndogo.

“Mheshimiwa mwenyekiti, Serikali ilitangaza msimu wa pamba ni tarehe moja mwezi Mei (kesho), lakini kwa sasa kuna walanguzi wamejazana wakipita kwa wakulima ambapo wananunua kilo moja kwa Sh500 hadi Sh600, je nini kauli ya Serikali kuhusu unyonyaji huu,” amesema Ndasa.

Bashungwa amesema msimu mpya unaanza kesho Jumatano na kwamba taratibu zote zimekamilika na Serikali na vikao imeshatoa mapendekezo yote.

Awali, Mbunge wa Nsimbo (CCM), Richard Mbogo alihoji ni lini Serikali itapeleka mbegu bora za tumbaku katika jimbo lake na lini itaruhusu kampuni nyingine za tumbaku kununua ili kuongeza ushindani.

Kuhusu kampuni za kununua, amesema Serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki kuongeza kampuni za ushindani.

Share.

About Author

Leave A Reply