Monday, August 26

Mpoto Band yanogesha ujio wa Sevilla Dar

0


By Thomas Ng’itu

Dar es Salaam. Bendi ya Mpoto leo ilitoa burudani wakati wageni wakisubiri kuwasili timu ya Sevilla inayoshiriki Ligi Kuu Hispania kwenye Uwanja wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Bendi hiyo ilianza kutoa burudani saa 1: 10 jioni ambapo msanii Ismail aliimba na baadaye wacheza sarakasi walinogesha kwa staili mbalimbali za uchezaji uliokonga nyoyo.

Pia wasanii waendesha baiskeli walitoa burudani kwa namna tofauti hatua iliyowapa raha watu waliojitokeza uwanjani hapo.

Pia kulikuwa na mwanadada ambaye alionyesha uhodari wa kucheza maringi kwa kutumia miguu na mikono hatua ambayo iligeuka kuwa kivutio.

Kivutio kingine alikuwa msanii wa kucheza na nyoka ambaye aliwashitua wageni waalikwa waliojitokeza uwanjani hapo kwa uhodari wake wa kucheza na nyoka wawili kwa namna tofauti.

Share.

About Author

Leave A Reply