Thursday, July 18

Mourinho abebwa na asiyempenda

0


Manchester, England. Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, jana alilazimika kumbeba kiungo asiyempenda katika kikosi chake Marouane Fellaini.

Mourinho alimkimbilia kiungo huyo kutoka Ubelgiji baada ya kumalizika mchezo kwa kufunga bao dakika ya kwanza ya muda wa ziada kuipeleka United 16 bora ya Ligi ya mabingwa Ulaya, baada ya kuishinda bao 1-0 Young Boys ya Uswisi.

Kabla ya kumbeba Fellaini, Mourinho alionekana kupagawa kuliko mtu yeyote uwanjani hapo kwani aliinua kreti ya chupa ya maji za kunywa wachezaji wake na kuipigiza chini.

Moja wa magwiji wa soka Uingereza, Gary Lineker, alisema kuwa kiasi kikubwa katika mchezo wa jana waliombeba Mourinho ni wale wachezaji asiowapenda akiwemo mshambuliaji kinda Marcus Rashford.

“Niliangalia namna Mourinho alivyopagawa baada ya lile bao kufungwa nikastaajabu kwa sababu aliyemfurahisha hivyo ni mchezaji ambaye yeye hampendi na amekuwa hampi nafasi ya kutosha kuisaidia timu,” Lineker.

Gwiji huyo ambaye ni mmoja wa washambuliaji wanaoheshima Uingereza, aliyepata kuzitumikia Leicester, Everton, Barcelona na Tottenham, alimtahadharisha kocha huyo kutobagua wachezaji.

Hata hivyo Mourinho raia wa Ureno, anasubiriwa na adhabu kutoka Shirikisho la soka Ulaya (Uefa) kwa kitendo chake cha kumwaga kreti la maji uwanjani.

Matokeo ya mechi zote za Ligi ya Mabingwa Ulaya zilizochezwa juzi   AEK Athens 0 Ajax 2, CSKA Moscow 1 Viktoria Plzen 2, Bayern Munich 5 Benfica 1, Lyon 2 Man City 2, Hoffenheim 2 Shakhtar Donetsk 3, AS Roma 0 Real Madrid 2, Juventus 1 Valencia 0, Man United 1 Young Boys 0.

Share.

About Author

Leave A Reply