Friday, July 19

Mo Rashid hana presha kutemwa CAF

0


By OLIPA ASSA

Dar es Salaam. Jina la Mohamed Rashid ‘Mo Rashid’ halijapelekwa CAF kuwa mmoja wa wachezaji watakaoichezea Simba katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, inayoanza Jumatano ya wiki hii dhidi ya Mbabane Swallows, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, hilo halimpi shida na kutamka kuwa anaendelea na mishe zake.

Mo Rashid anasema amechukulia jambo la kawaida kutojumuishwa kwenye majina ambayo yamepelekwa CAF na viongozi wa Simba na kudai kuwa muda timu  inacheza michuano hiyo yeye ataendelea na programu zake za mazoezi.

“Unapokuwa mchezaji lazima utambue kwamba kuna kung’ara na changamoto, ni kweli hakuna mchezaji asipenda kucheza michuano ya CAF, lakini inapotokea umekwama inakubidi kutafuta njia ya kufanya kiwango chako kiwe juu.

“Uzuri na programu zenyewe nimepewa na kocha Patrick Aussems ambayo nitakuwa nafanya timu ikisafiri nje, lakini wakiwa Dar es Salaam nafanya na timu, nimejipanga popote nitakapokuwepo ndani ya msimu huu nifanye kitu cha pekee,” anasema.

Tangu ajiunge na Simba mwanzoni mwa msimu huu, akitokea Prisons ambako alimaliza akiwa na mabao tisa, Mo Rashid amesema uwepo wa Emmanuel Okwi, Meddie Kagere na John Bocco unafanya asiwe na nafasi ya kucheza.

Share.

About Author

Leave A Reply