Wednesday, August 21

Mo, Ndugai watoa neno zito Tuzo za Mo Simba Awards

0


By Thobias Sebastian

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ amewasihi wachezaji wa timu hiyo kutambua ukubwa wa klabu yako.

Mo Dewji alisema wachezaji, viongozi na benchi la ufundi wanatakiwa kutambua ukubwa na thamani ya klabu hiyo.

“Wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wanatakiwa kupambana Kadri wanavyoweza ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika kila mechi,” alisema Mo.

“Mimi mwenyewe nikiwa pale uwanjani muda mwingine mkono huwa inatetemeka na kufa gazi pindi timu inaposhindwa kufanya vizuri inakuaje kwa wale mashabiki wengine.

“Kwahiyo wachezaji wanatakiwa kuelewa na kufahamu maumivu ambayo wanayapata wapenzi na mashabiki wa timu yetu.

“Ndio maana tumewawekea tuzo hizi ili kupanda kupambana na kufikia yale malengo kw maana ya kupata matokeo mazuri mara kwa mara,” alisema Mo Dewji.

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amewapa neno viongozi wote wa Simba katika kipindi hiki cha usajili.

Ndugai mgeni rasmi wa tukio hili aliwambia viongozi wa Simba wanatakiwa kufanya usajili n wenye Nguvu katika kipindi hiki.

“Simba walipofiki msimu huu katika mashindano ya kimataifa wametubeba Tanzania na ili kufanya vizuri zaidi wanatakiw kufanya usajili wa maana,” alisema Ndugai.

“Tumeona mapungufu mengi haswa katika michezo ya kimataifa ambayo tulifungwa mabao mengi msimu huu viongozi inatakiwa kuweka umakini na akili katika kupata wachezaji wapya wa maana,” alisema.

“Naimani tukifanya usajili mzuri tutaweza kufika mbali zaidi ya msimu huu kwahiyo viongozi wote mnatakuwa kuongeza wapya waana,” alisema Ndugai.


Share.

About Author

Leave A Reply