Friday, July 19

Mkutano wa EAC waahirishwa kwa kukosekana Nkurunzinza

0Akitoa taarifa ya kuahirishwa kwa mkutano huo Mwenyekiti wa baraza la Mawaziri wa nchi hizo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Augustino Mahiga, amesema koram ya mkutano ilikuwa haijakamilika.

Wakizungumza baada ya kuahirishwa kwa mkutano huo baadhi ya washiriki akiwemo mkurugenzi wa baraza la biashara la Afrika Mashariki Peter Mathuki amesema kuahirishwa huko hakuna athari kubwa katika sekta ya biashara.

Mkutano huo wa viongozi pamoja na masuala mengine ulikuwa ujadili mapendekezo ya kusuluhisha mzozo wa Burundi, yaliyo fikishwa na mpatanishi mkuu wa mzozo huo Rais Yoweri Museveni wa Uganda.

Share.

About Author

Leave A Reply