Tuesday, August 20

Miller avunja pambano lake na Joshua kinamna

0


Dallas, Marekani. Siku za karibuni, kumeandaliwa mpambano wa makonde kati ya bondia Jarrell Miller na Anthony Joshua lililokuwa lifanyike Juni Mosi, lakini Miller ni kama amelivunja kwa staili yake.

Mpambano huo ulikuwa ufanyike kwenye mji wa New York, Marekani Juni Mosi lakini matatizo yalianza Machi 20 wakati Taasisi ya Voluntary Anti-Doping Association (VADA), ilimpima na kumkuta akiwa na vimelea vya dawa za kusisimua misuli zilizopigwa marufuku.

“Nimeumizwa sana kusikia leseni yangu ya ngumi imesitishwa na Jimbo la NY na kiukweli nitakata rufani katika hili,’ Miller aliandika kwenye Mtandao wake wa Instagram kuhusiana na tuhuma hizo.

‘Sikuwahi wala sikuwa na mpango wa kutumia dawa ilizokatazwa, kwa kweli nilipoona habari hizi, zilinishtua sana,” alisema.

Alisema: ‘Mimi pamoja na watu wangu tunasimamia kwenye weledi, umakini na ukweli na kwa pamoja tutasimama kupignga hili. “Nilichukuliwa vipimo kwa hiari na ni mara ya pili, mara ya kwanza ilikuwa safi na mara ya pili majibu yakawa ovyo,” alisema.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa mpinzani huyo wa Joshua, mwenyewe (Joshua) alisema anatafuta pambano mbadala kwa kuwa alikwishaanza maandalizi na gharama nyingi ameshatumia kujiandaa pambano lililofutwa.

Share.

About Author

Leave A Reply