Friday, August 23

Mbunge CCM adai makato mikopo elimu ya juu makubwa

0


By Sharon Sauwa, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Mbunge Viti Maalum (CCM), Dk Jasmin Tisekwa ameishauri Serikali kupitia upya mikopo ya elimu ya juu kwa sababu asilimia 15 ya makato kwa waliopewa mikopo hiyo ni kubwa hasa kwa wanaotokea familia duni.

Akizungumza katika mjadala wa najeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  ya mwaka wa fedha 2019/2020 bingeni leo, Dk Tisekwa amesema asilimia 15 ni kubwa na kama inawezekana ipitiwe upya.

“Kwa sababu anayeenda kulipa katika kazi anayoifanya anatoka familia masikini kwahiyo bado unambebesha tena asilimia 10 ya faini akichelewa kulipa,” amesema.

Amesema mbali na faini, mnufaika huyo pia anatakiwa kulipa kodi nyingine na bado anakatwa rejesho la asilimia 15.

Amesema katika mikopo ya halmashauri Serikali imeondoa makato na kuhoji kwanini na katika mikopo ya elimu ya juu isiondoe.

Hata hivyo, amesema wanufaika wa mikopo hiyo wanapongeza hatua ya Serikali kuanzisha utaratibu wa alama za vidole (finger print) lakini wanalalamikia kuchelewa kupata mikopo yao.

Amesema wanufaika hao wanaipongeza Taasisi ya Mikopo ya Elimu ya Juu  makao makuu lakini wanasema tatizo bado liko katika ofisi za kanda.

Share.

About Author

Leave A Reply