Sunday, August 25

Mbunge ashangaa kukamatwa mtu mmoja matukio ya mtekaji

0


By Habel Chidawali, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Mbunge wa Wingwi (CUF), Juma Kombo Hamadi ameshangazwa na majibu ya Serikali kwamba hadi sasa imemkamata mtu mmoja tu anayeshukiwa kwa matukio ya utekaji.

Hamad amesema yapo matukio mengi ya utekaji, kuwatesa hata kuwaua raia wasiokuwa na hatia lakini na kushangazwa kuwa hadi sasa anatajwa mtuhumiwa mmoja kuhusika.

“Kuna matukio mengi likiwamo la Tundu Lisu, Mohammed Dewj lakini mtaa wa Mtambwe kule vijana saba walitekwa na matukio mengi halafu mnasema anashikiliwa mtu mmoja,” amehoji Hamad ndani ya bunge leo Alhamisi Aprili 25.

Katika swali la msingi amehoji Serikali watu wangapi wanashikiliwa hadi sasa kwa matukio hayo.

Akijibu, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema jukumu la msingi la Serikali ni kuhakikisha raia wake wanakuwa salama wakati wote.

Amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali inapopata taarifa za utekaji, utesaji ama mauaji.

Hamad amesema kwa kutumia taarifa za kiintelejensia hadi sasa imefanikiwa kumkamata mtu mmoja kwa makosa ya utekaji nyara.

Share.

About Author

Leave A Reply