Sunday, August 25

Mbonde atoa neno mechi ya Njombe Mji

0


Beki wa Simba, Salim Mbonde amesema wanatakiwa kuwa makini ni pale wanapokutana na timu zinazokuwa zinajikwamua na kushuka daraja.

Mbonde aliyeanza mazoezi na wenzake baada ya kupona majeruhi alitoa kauli hiyo wakati Simba ikijiandaa na mechi yake dhidi ya Njombe Mji, itakayopigwa Aprili 3,Uwanja wa Sabasaba.

Wengi wanaona Simba watapata mtelemko, lakini beki huyo ameitazama kwa jicho la pekee, kuona wanahitaji kujipanga ili wapate pointi tatu muhimu.

“Kwanza tukishinda itatutofautisha pointi na Yanga, ambao wamecheza mechi 21 sisi 20, itatulazimu¬† tuichange vizuri karata zetu ili tufikie malengo,”

“Nimejifunza tunapokutana na timu za mkoani, zinakuwa zinaikamia sana Simba ama Yanga, lengo ni wachezaji kutaka kupata ulaji ndani ya klabu hizo, hilo ni jambo litakalotufanya tuwe makini zaidi na huo mchezo,” alisema Mbonde.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.