Wednesday, August 21

Mbinu, ufundi vyakosekana Yanga, Azam Uwanja wa Taifa

0


By Olipa Assa

Dar es Salaam. Pamoja na Azam FC kushinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Yanga, wachezaji wa timu hizo walicheza kwa kupooza tofauti na walivyokutana kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza.

Bao pekee la Mrisho Ngassa liliwafanya Yanga kushinda mechi ya mzunguko wa kwanza na mechi ilikuwa na ushindani wa hali ya juu tofauti na ya leo.

Hata hivyo mechi ya leo, hakuibadilisha chochote kwani hata matokeo Azam FC kushinda mabao 2-0 watabakia nafasi ya tatu na Yanga ya pili.

Ni juhudi ya mchezaji mmoja mmoja lakini sio kucheza kitimu si kwa Yanga wala Azam FC.

Kwa upande wa Yanga kuingia kwa Amissi Tambwe kipindi cha pili kumeongeza uhai safu yao ya ushambuliaji baada ya kuchukua nafasi ya Gustapha Simon.

Tambwe alionekana kuwapa kazi mabeki wa Azam FC kuokoa shuti zake kwani anapambana na kuonyesha uhitaji wa kuzifumania nyavu.

Obrey Chirwa wa Azam FC anaonekana kupambana huku akimpindua pindua beki wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ambaye anaonekana kupata shida kupambana naye.

Mbinu, ufundi na kasi vinaonekana kukosekana katika mchezo wa leo huku kukiwa hakuna mchecheto kwa makocha kuonekana kuwaelekeza wachezaji wao.


Share.

About Author

Leave A Reply