Monday, June 24

Mbeya City chupuchupu kwa Lyon

0


By OLIPA ASSA

SARE ya bao 2-2 waliyoipata Mbeya City dhidi ya African Lyon jana Jumamosi, imewapandisha mpaka nafasi ya saba, ikiwa sawa pointi 47 na Ndanda FC isipokuwa tofauti ya mabao.
Kabla ya mchezo huo, Mbeya City ilikuwa na pointi 46 na mabao 36, Ndanda FC wao wana pointi 47 na  mabao 23, hilo ndilo linalowapa nafasi City kupanda nafasi ya saba na Ndanda kushuka ya nane.
Lyon ndio iliyokuwa imetawala mchezo na ilifanikiwa kupata mabao 2-0 katika kipindi cha kwanza ambapo City ilipata shida kusawazisha kipindi cha pili.
Mpaka sasa City wanamiliki mabao 38 na wamefungwa mabao 38 bao lao la pili dhidi ya Lyon ilipata dakika za nyongeza, hii inaonyesha jinsi ambavyo mechi ilikuwa ngumu kwa upande wao.
Kwa upande wa Lyon, hawana chakupoteza kwa kuwa tayari wameishashuka daraja kutokana na kile ambacho wamekivuna katika mechi 36 walizocheza, wameshinda nne, wametoka sare 11, wamefungwa 21, wanamiliki pointi 23 mpaka sasa.
Hata ikishinda mechi zao mbili zilizobakia haziwezi kuwasaidia chochote kwani watafikisha jumla ya pointi 29.

  


Share.

About Author

Leave A Reply